Rushwa ni kama Pweza – Reginald Mengi

Mfanyabiashara na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Limited, Dkt. Reginald Mengi amewaasa Watanzania kuwa wakati tunapambana na rushwa ni vyema tukatumia nguvu na muda mwingi katika mapambano lasivyo itakuwa ngumu kuitokomeza.
Dkt. Mengi amefananisha mapigano dhidi ya Rushwa kama mapambano ya mvuvi na samaki aina ya Pweza kwa kusema ili uweze kupambana nae huna budi kuongeza nguvu ya ziada pamoja na muda mrefu hadi kuja kumuangamiza.

Tunapo andaa mikakati ya kutokomeza rushwa, tukumbuke rushwa ni kama pweza, kumuua lazima umpige kwa nguvu na kwa muda mrefu”,ameandika Reginald Mengi kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Hata hivyo kwa sasa Serikali ya awamu ya Tano imejitahidi kupambana na vitendo vya rushwa na kufanikiwa kiasi hususani kwenye taasisi za umma ukilinganisha na awamu zilizopita.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment