Safari ya AY kuingia kwenye maisha ya ndoa yaanza kunukia

Weekend hii tulishuhudia tukio la kihistoria la msanii mkongwe wa hip hop, Joseph Haule aka Professor Jay ambaye ni mbunge wa jimbo la Mikumi, akifunga ndoa na mpenzi wake wa zamani aitwaye, Grace Mgonjo.

Tukio hilo la aina yake lililowakusanya mastaa wa muziki pamoja na wabunge lilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.

AY akiwa kwenye ndoa ya Professor Jay pamoja na mtu wake wa karibu.
Bongo5 ilipata nafasi ya kuzungumza na Black Rhyno ambaye ni mdogo wa Professor Jay, ambapo aliizungumzia ndoa hiyo pamoja na ishu ya yeye kuoa kabla ya kaka yake.
“Hii ni habari njema kwa sababu binafsi kila siku nilikuwa namwambia broo Jay oa kwa sababu mimi nimeoa miaka 5 nyuma na mpaka sasa bado nipo sawa. Pia nadhani alikuwa anajipanga zaidi ndio maana amechelewa kidogo lakini siwezi kusema amechelewa labda huu ndio wakati wake sahihi wa kuoa kwa sasa, muda uliopita nilikuwa naongea na AY hapa akawa ananiambia na yeye soon anafunga ndoa na mpenzi wake. Kwa hiyo mimi naweza kusema kila kitu kinakuja kwa wakati,” alisema Black Rhyno.
Rapa huyo amedai yeye maisha yake yamepiga hatua zaidi baada ya kuoa huku akidai huwenda angeshindwa kufanya baadhi ya mambo kama angekuwa single.
Ndoa ya Professor Jay ilihudhuriwa na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe pamoja na Waziri mkuu wa zamani wa Tanzania, Edward Lowassa.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment