Shamsa Ford wachana wanaume wanaopenda kulelewa,auliza hawaumii kwa majina kama VIBENTEN,VIPANYABUKU,VICHURA wanavyoitwa

Msanii wa Filamu nchini, Shamsa Ford amewatolea uvivu wanaume wanaopenda kulelewa na wanawake.

Kupitia mtandao wa Instagram muigizaji huyo ameonyeshwa kukerwa na tabia hiyo ambayo inapekea wawe tegemezi kwa wapenzi hao kutokana na kuchagua kazi.
“Kaka zangu na wadogo zangu wa kiume ningependa kuwashauli mpende kujituma na kufanya kazi kwa bidii, usitamani kazi ya kuzunguka kwenye kiti ofisini wakati elimu yako ni darasa la pili. Mwanaume unatakiwa ujitume na kupambana na maisha, sukuma hata mkokoteni ilimradi ujipatie riziki.,” ameandika mrembo huyo.
Akaongeza “Sasa nyie kaka zangu wa sasa hivi yaani hampendi kufanya kazi ukishajiona una sura nzuri basi na wewe eti unadanga kwa jimama lenye pesa. Sasa kama mwanamke anakufuga wewe unadhani atakuheshimu?utachezea kuchapwa vibao na kutukanwa, hivi hamuumii na haya majina mnayoitwa?mara vibenten,vipanyabuku,vichura,vitom and jerry…daah.”
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.