Shilole Asema kashatolewa hela ya barua, kuolewa muda wowote

Muimbaji Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amedai ameshatolewa barua na mpenzi wake aliyenaye kwenye mahusiano na endapo Mungu akimjalia atafunga naye ndoa ili kuhalalisha.

Shilole amedai kwa sasa ameamua kuweka mahusiano yake faragha kidogo ili aweze kuwa huru na mpenzi wake.

“Mimi kwa sasa hivi sina boyfriend kabisa, niwaambie tu nina mchumba ambaye tayari ameshanitolea mpaka barua, Mungu akijaalia harusi nitawakaribisha siku siyo nyingi. Na kuhusu wapenzi waliopita kuwa na mahusiano na marafiki zangu naona ni kitu cha kawaida kwa sababu naamini mapenzi ni kama daladala ukishuka mwenzako anakaa” Shishi alikiambia kipindi cha 5Selekt ya EATV

Kuhusiana na muziki wake msanii huyo amedai anashindwa kutoa wimbo mpya kutoka na akaunti yake ya mtandao wa instagram kudukuliwa na wahalifu wa mtandao.

“Nina miezi mitano tangu nimeachia wimbo wa hatutoi remix najua masabiki zaingu wamenimiss sana lakini kinachonifanywa nishindwe ni kuwapa taarifa mashabiki zangu. Dunia sasa ipo mikononi mwa watu na kwa wasanii inatusaidia kusukuma kazi zetu ” aliongeza.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.