Vicent Mashinji na wabunge wawili wa CHADEMA waswekwa rumandeViongozi tisa wa Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) wakiwemo Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt. Vicent Mashinji na Wabunge wawili wamewekwa ndani huko mkoani Ruvuma kwa masaa 48 kutokana na kile kinachodaiwa kuwa wamefanya mkutano bila kibali maalum.


Mhe. Dkt. Vincent Mashinji

Taarifa iliyotolewa na CHADEMA inasema kuwa Mkuu wa Polisi wa wilaya (OCD) wa Nyasa amedai amewaweka ndani viongozi hao jana jioni kutokana na maagizo aliyopewa.

“Katibu Mkuu wa Chama Dr. Vincent Mashinji pamoja na viongozi wengine 8 wa chama wakiwemo wabunge wawili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamewekwa ndani kwa masaa 48 kwa kile ambacho OCD wa Wilaya ya Nyasa amesema ni maagizo aliyopewa” Imeeleza Taarifa iliyotolewa na CHADEMA.

Majina ya waliokamatwa ni Mhe. Dr. Vincent Mashinji (Katibu Mkuu), Mhe. Cecil Mwambe (M/kiti wa Kanda na Mbunge wa Ndanda), Philbert Ngatunga (Katibu wa Kanda), Ireneus Ngwatura (Mkiti Míos), Delphin Gazia (Katibu Mkoa), Zubeda Sakuru (Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma), Asía Mohamed (Afisa Kanda), Cuthbert Ngwata (Mkiti Wilaya) na Charles Makunguru (Mwenezi Wilaya).

Awali viongozi hao walikamatwa na kwenda kuhojiwa kwa kufanya mkutano kinyume na sheria na utaratibu lakini baadaye waliwekwa ndani na kutakiwa kukaa masaa 48 kutokana na kukaidi maagizo waliyopewa.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment