Wachezaji wa Everton watembelea shule ya Uhuru Mchanganyiko ,

Baadhi ya wachezaji wa Klabu ya Everton iliyowasili leo Jumatano asubuhi ikitokea Uingereza, wametembelea Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko iliyopo jijini Dar es salaam na kushiriki michezo tofauti tofauti na watoto wenye ulemavu wa Usikivu na Uoni  hafifu.

Idrissa Gueye na wachezaji wenzake wakipokewa naWanafunzi wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko

Wachezaji walioshiriki na watoto hao ni Leighton Baines, Idrissa Gueye na Ademola Lookman walijionea vifaa mbalimbali vinavyotumiwa na Watoto hao kwa kujifunzia ambavyo vimetolewa na Shirika la Misaada la (UK Aid).


Wachezaji hao wakiwa wamefunikwa nyuso zao kwa vitambaa maalumu na kuzibwa masikiok na macho yao, walicheza na watoto wenye ulemavu michezo mbalimbali ikiwemo soka ili kujionea ugumu waupatao watoto hao kwenye maisha yao ya kila siku.


“Sisi wote pale Everton tunatambua umuhimu wa shule na ni furaha yetu kuona  UK aid ikisaidia Watoto hapa Tanzania. Kila mtoto anastahili kupata nafasi ya kusoma kwa ajili ya maisha yake ya baadae .Mpira wa miguu pia ni njia nzuri ya kujifunza namna ya kufanya kazi pamoja kama familia,“amesema Leighton Baines.


Timu ya Everton ipo nchini Tanzania kucheza mechi ya kirafiki na Washindi wa michuano ya Sportpesa Super Cup, Gor Mahia kutoka nchini Kenya mchezo ambao utafanyika LEO alhamisi (julai 13) majira ya saa 11 jioniShare on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment