Alikiba sio ‘Kipusa’ tena, ni ‘Seduce Me’ New Video

Msanii wa muziki kutoka RockStar4000, Alikiba ameachia wimbo wake mpya uitwao’Seduce Me’.
Muimbaji huyo alikuwa kwenye promotion za ujio wake mpya wiki hii hali ambayo iliibua gumzo mtandaoni huku wengi wakidhani ataachia wimbo ‘Kipusa’ baada ya kuonekana analitumia sana neno hilo katika ujio huo.

Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa muimbaji huyo amesema leo ataachia wimbo wake huo kupitia vituo vya runinga pamoja na channel yake ya YouTube.
“#SeduceMe Exclusive Premiere Tomorrow 25.08.2017 on AlikibaVEVO & Global Music Stores
Subscribe now on AlikibaVEVO.#RockstarTV #SHOOOOSH #SonyMusicAfrica #RockStar4000 #KingKiba,” aliandika Alikiba Facebook.

Kitendo hicho kimewavutia zaidi mashabiki wa muziki wake ambao wameusubiri ujio huo kwa zaidi ya mwaka mmoja toka aachie wimbo Aje ambao ulifanya vizuri kila sehemu.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment