Amber Lulu akipelekwa kituo cha Polisi cha Urafiki kisa picha chafu

Msanii wa muziki na video vixen, Amber Lulu Jumanne hii alipelekwa kituo cha polisi cha Urafiki Ubungo jijini Dar es salaam kueleza kama anahusika katika kusambaza picha chafu mtandaoni ambazo zinamuonyesha akiwa nusu uchi na rapa Young Dee.


Amber Lulu akiingia kituo cha polisi cha Urafiki Ubungo jijini Dar es salaam hapo jana.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo tumezipata, zinadai kwa sasa muimbaji huyo yupo nje baada ya kuhojiwa kwa masaa machache kuhusiana na tukio hilo.
Akiongea na Bongo5 Jumaatano hii shuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema mrembo huyo alishikiliwa na kituo hicho kwa masaa matatu na baada ya hapo aliachiwa.
“Ni kweli Amber Lulu alikuja na tulimuona hapa kituoni jana kama jioni jioni hivi,” alisema shuhuda huyo ambaye hakutaka atajwe jina lake.
Shuhuda huyo alidai mrembo huyo alifika kituoni hapo akiwa na team yake ya uongozi kutoka Afrika Kusini pamoja na uongozi wa Young Dee.
Bongo5 ilimtafuta meneja wa Young Dee ili kuzungumzia sakata hilo lakini meneja huyo hakuwa anapokea simu hata hivyo alivyotumiwa meseji alisema bado wanalishughulikia tatizo hilo na pale watakapokuwa na taarifa rasmi wataitoa kwa jamii.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.