BAADA YA KUKOSEWA MANENO KWENYE NGAO YA JAMII, TFF WAZUNGUMZA HAYA;

Kufutia kukosewa kwa neno kwenye Ngao ya Jamii siku ya Jana, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeomba radhi wanafamilia wote wa mpira wa miguu kutokana na makosa hayo yaliyoonekana kwenye utambulisho wa Ngao ya Jamii iliyotolewa Jumatano Agosti 23, 2017.

Ngao hiyo ilitolewa mara baada ya mchezo uliokutanisha timu za Simba SC na Yanga SC kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa jijini Dar es salaam Mchezo ambao Simba iliibuka na ushinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya Yanga na kutwaa Ngao hiyo.
Baada ya Makosa hayo Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, tayari amechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi waliohusika kadhalika kuwasiliana na uongozi wa Simba SC kuirejesha Ngao hiyo ili kufanyiwa marekebisho yatakayobaki kwenye kumbukumbu sahihi. Pia TFF imetoa taarifa kuwa suala hilo haliwezi kutokea wala kujirudia tena.
Ngao ya hisani hiyo ilikosewa neno Ngao kwa lugha ya kiingereza ambalo liliandikwa “Sheild” badala ya “Shield” ambalo wadau na Mashabiki mbalimbali wa Soka nchini hawajapendezewa nayo kwa kuona ni kosa ambalo linaonyesha kukosekana kwa umakini ndani ya TFF.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment