Dulla Makabila na Husna Sajent mapenzi mubashara, ndoa mbioni

Msanii wa muziki Singeli, Dulla Makabila na msanii wa filamu Bongo Husna Sajent mapenzi yao wamepamba moto kiasi kwamba kuweka wazi kufunga ndoa.

Dulla amesema mapenzi yao yalianza miezi saba iliyopita ila hawakutaka kuweka hadharani ila kwa sasa kwa vile wanaishi pamoja na kila mmoja amemridhia mwenzake wameamua kuweka wazi.
Ameongeza kuwa yupo tayari kuwalea watoto wawili wa Husna na ni jambo ambalo familia inalitambua.
“Ni kweli kwa sababu wahenga hawajaacha kitu wanakuambia ukipenda boga unapenda na ua lake, nashukuru watoto wananipenda na mimi nawapenda na ninaweza kuwahudumia, familia zimeridhia ndio maana tupo wote,” ameiambia E-Newz ya EATV na kuongeza.
“Tunaishi tunaheshimiana, huwezi ukaamini tangu niishi na Husna kama aliniboa sijui kama inafika hata mara tano. Muda mwingi sana tumekaa pamoja, hatukuchua muda mrefu tukaanza kusihi wote, tulikaa kama miezi miwili, alikuja home akanogewa basi akasahau kwake, hivyo yaani,” amesema Dulla Makabila.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment