Elizabeth Michael atamfundisha binti yake kwamba uzuri/muonekano sio kitu cha kujisifia bali kushukuruSometimes Lulu huwa anakua na ujumbe mzuri sana wakufundisha ,sio kwa wale wa umri mdogo tu bali hata watu wazima,
Anasema akijaaliwa kupata mtoto wa kike atamfundisha kutokutegemea uzuri wake kupata maisha mazuri,au vitu anavyohitaji bali kwa kufanya kazi,kusoma nk kuongeza thamani yake.
Amepost mengi baada ya mwigizaji wa Ki Nigeria kuandika hivi kwenye ukurasa wake,kwamba atawaeleza watoto wake kwamba uzuri sio kila kitu lazima wafanye kazi kwa bidii.
Hii ni ile wasichana wengi wanaoishi kutegemea uzuri wao au miili yao.

What A coincidence....Niliwahi kuwaza hivi Pia...!
Siku Nikijaaliwa kupata Mtoto(Hasa wa kike)Nitamfundisha KUSHUKURU kwa Muonekano aliopewa Na sio Kujisifu au Kuhisi Muonekano wake unaweza kumsaidia kupata kitu chochote katika maisha yake.....!
.
.
Binafsi Naonaga Muonekano/Uzuri/Urembo sio kitu cha kujisifu Maana sio kitu Unique(kitu cha kipekee)
Unaweza kuwa Mzuri Dar na ukienda Dar hii hii ukakuta wazuri wengine wengi tu,hapo hujatoka nje ya dar,nje nchi,nje Bara ukakutana na wengine Tena...sooo There's nothing special there...!
Nadhani Kama Wewe ni Binti/Kijana mwenye muonekano mzuri ni Jambo La kushukuru na sio KujifisušŸ˜ŠIla unaweza kuwa wa kipekee Kwa kuongeza kitu/vitu ndani yako zaidi ya Muonekano...Kama ni kwa Kusoma,Kufanya Kazi au chochote kile kinachoweza kukupa thamani zaidi na utofauti kati ya Wazuriiii Weeengiii Duniani

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment