HARUFU YA CHANDA CHEMA KUVISHWA PETE YANUKIA KWA DIAMOND PLATNUMZ NA MPENZIWE ZARI

Staa wa ngoma ya ‘Eneka’ Naseeb Abdlu a.k.a Diamond Platnumz ameonesha dalili za kupiga hatua ya mahusiano yake na mpenzi wake Zari The BossLady aliyewasili Tanzania siku ya Jumamosi ya wiki iliyopita.  Kupitia mtandao wa Instagram akaunti ya Diamond Platnumz siku ya jana alipost kipande cha video kilicho sambamba na msikiko wa wimbo ‘Malaika’ wa Nyashinski kutoka Kenya kipande kinachonesha pambo la michoro ya ‘Hina’ kwenye miguu na mikono wa kushoto wa Zari ukiwa ni wenye pete katika kidole cha chanda(Inahisiwa kuwa sasa ni muda wa chanda chema kuvishwa pete).


Hata hivyo katika hili inaoneaka kuwa kuna kila dalili za kufanyika kwa hatua kubwa ya kimahusiano kwa wawili hawa kwakuwa hili linaweza kutafsiriwa kuwa ni jambo lililoko nyuma ya safari ya kuja kwa Zari nchini Tanzania mara hii kwakuwa limetokea ndani ya muda mfupi tangu kufika kwake.
Itazame video nzima iliyonaswa ya Dizmond Platnumz akimpokea Zari Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jumamosi ya tarehe 26.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment