Jux akumbuka penzi la Vanessa Mdee, amuandikia ujumbe mzito

Inauma sana mtu ambaye mumezoea na kuchangia kila kitu kwa pamoja kuona ghafla haupo naye. Hilo ndio jambo linaonekana kumtesa Jux kwa sasa baada ya kuvunjika kwa mahusiano yake na Vanessa Mdee.

Msanii huyo ambaye Ijumaa hii anasherekea siku yake ya kuzaliwa, ameandika ujumbe mzito kwa ex wake huyo kupitia mtandao wa Instagram. Kupitia mtandao huo Jux ameandika:
Nakumbuka mara ya mwisho kufanya party ya Birthday yangu ilikuwa 2013, Miaka
minne iliyopita. Sikuwahi kufanya party yoyote tena sababu nilikuwa na rafiki, mpenzi na mtu wa karibu kuliko mtu yoyote kwenye maisha yangu. Miaka yote iliyofata nilikuwa na yeye mpaka sasa atuko tena karibu kama mwanzo, Tumebaki kuwa marafiki wa kawaida tu ๐Ÿ˜”๐Ÿ˜”๐Ÿ˜”. Uwepo wake tu ulikuwa ni zaidi ya chochote kwenye siku yangu ya kuzaliwa, Kuongea na yeye au txt yake tu ilitosha kukamilisha siku yangu. Ila sasa sidhani kama itakuwa kama mwanzo ๐Ÿ˜”๐Ÿ˜”๐Ÿ˜”. Nitafarijika sana kama nitamuona hiyo siku. This time nataka kuparty na watu wangu nani anataka kuparty na mimi katika siku ya birthday yangu ?
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.