Kesi ya Wema kusomwa mara 2 leo mahakamani

Kesi ya malkia wa filamu nchini Wema Sepetu imesogezwa mbele Jumatatu hii

Kesi hiyo inayosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajiwa kusikilizwa tena majira ya saa sita na nusu mchana leo baada ya Wakili wa upande wa utetezi kushindwa kufika mahakamani kutokana na kupata dharura.
Aidha Hakimu anayesikiliza kesi hiyo alipanga kuisogeza mbele mpaka Alhamisi ya wiki hii lakini Wakili wa upande wa serikali alidai kama kesi hiyo haitaweza kusikilizwa tena leo haitawezekana kupata ushahidi kutoka kwa Mkemia Mkuu kutokana na kubanwa na safari nyingi.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment