Lucy Komba awatolea povu Watanzania wanaomponda Mobetto kisa Zari

Msanii wa filamu, Lucy Komba amewatolea uvivu Watanzania katika mitandao ya kijamii ambao wanamponda mtanzania mwenzao, Hamisa Mobetto kisa mama watoto wa Diamond, Zari The Bosslady.

Mobetto ambaye ni mwanamitindo maarufu nchini, wiki iliyopita alijifungua mtoto wa kiume ambaye baba yake hakutambulika mara moja. Lakini tetesi ambazo zinazunguzwa kwenye mitandao ya kijamii ni kwamba mtoto huyo ni wa Diamond hali ambayo imezua hataruki kati ya timu Zari na timu, Mobetto.
Ukweli wa yote anaujua mwanamitindo huyo lakini katika mitandao ya kijamii kimezuka kikundi ambacho kinajiita ni timu Zari na kuamua kumtukana Mobetto hali ambayo imemfanya muigizaji, Lucy Komba ambaye anaishi nchini Sweeden ashindwe  kuvumilia na kuamua kuingilia kati sakata hilo.
“Samahani lakini kimenichoma. MABOGAS YA TZ YANAMPONDA MTZ MWENZIO YANAMSIFIA BOGAS MWENZIO sijui yanafikiri yatapewa ule urithi. Mbona waganda hawambabaikii acheni umasikini wa kujirahisisha. Au mnafikiri mtapitishiwa kila mmoja karanga moja moja ya bure,” aliandika Lucy Komba Instagram.
Aliongeza, “Hongera mwanamke mwenzangu, wanajifanya roho ngumu tu kukuponda wakati roho zinawauma unatoa vitu hasa mwanamke unazaa huku unatabasamu ☺. Wale wanaoniponda eti ningekuwa mzalendo nisingeolewa na mzungu, Yes nimeolewa na mzungu sababu sina ubaguzi wa rangi wala ukabila na tangu nimeolewa sijawahi kutukana kaka zangu wakisfrika kwa hiyo lazima mjue kutofautisha A na B. Pili anayewapa taarifa nimeachwa nahisi kama kachelewa kuwataharifu halafu mwambieni awape taarifa kamili maana huwa anaingia insta na kuzizungusha bado hajawapata taarifa za kunichamba huku mmesimaisha visimi ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚. Ukweli unauma mmepewa ukweli wa huyo stranger wenu aliyenenepesha miguu kiuno kimeshindikana kukipunguza mnalia chambeni tu mniongezee followers maana nilikuwa sijaamka bado kujua kumbe umaarufu wa bongo unatokana na vichambo ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚GOODMORNING.,”
Mpaka sasa bado mwanamitindo huyo hajaweka wazi kwamba mtoto huyo ni wa nani. Pia huyo ni mtoto wa pili ambapo  wa kwanza alizaa na Mkurugenzi wa EFM, Majay.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment