MCT yaeleza RC Makonda alivyowakwepa sakata la Clouds

Baraza la Habari Tanzania (MCT), ilisema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia studio za Clouds Media Group (CMG) imeonyesha jinsi kiongozi huyo alivyowakwepa timu ya uchunguzi na kukosa kupata maelezo ya upande wake.

Ripoti hiyo iliyosomwa jana Mwanasheria mwandamizi, Juma Thomas ambaye ni Mwenyekiti wa kamati iliyokuwa na watu wanne, amesema Kitendo cha Makonda kwenda kwenye kituo cha Clouds Media ni kukiuka na kinyume cha Huduma za vyombo vya habari.
“Timu ilifanya juhudi za kukutana na Mkuu wa mkoa lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda, tulienda mara nyingi sana ofisini kwake lakini tumekuwa tukifika tunaambiwa ana shughuli nje ya ofisi tuliandika barua lakini hatukujibiwa kwahiyo ile right ya kureply tuliyompa hatukuitumia kwahiyo ikabidi tuandike ripoti bila ya kuwa na input yake.”
“Barua hiyo yenye kumbukumbu namba MCT/15/005/2017 iliandikwa Mei 2 na ilipokelewa na kugongwa mhuri wa mkuu wa mkoa Mei 4 lakini mpaka ripoti hii inaandikwa, barua hiyo haikuwa imeshughulikiwa,” ilisema ripoti hiyo.
“Licha ya kutuma barua hiyo, timu ya MCT ilifika mara tatu katika ofisi ya Mkuu wa mkoa na mara zote iliambiwa kuwa ratiba ya Bw Makonda ilikuwa imebanwa na alikuwa na mambo mengi yaliyomtinga.”

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment