Migogoro na serikali ilianza baada ya kutoka CCM – Sumaye

Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye amesema kuwa alitoka CCM na kujiunga Chadema kwa hiari yake mwenyewe na maslahi ya umma huku akisema kuwa migogoro yake na serikali ilianza tangu yeye alipotoka CCM.

Akizungumza na wanahabari leo, Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye amesema wakati natoka CCM mwezi Agosti 2015 nilieleza kwa ufasaha sana kwanini ninatoka CCM na kujiunga Upinzani.
“Mimi nilitoka CCM na kujiunga na Chadema kwa hiari yangu mwenyewe kwa maslahi ya umma , wakati natoka CCM mwezi Agosti 2015 nilieleza kwa ufasaha sana kwanini ninatoka CCM na kujiunga Upinzani. Labda nirudie kwa ufupi labda hata wanaonifungia visasi wakielewa wanaweza kunipongeza badala ya kuniumiza,” amesema Sumaye.
“Migogoro yangu na serikali ilianza mara tu baada ya mimi kutoka CCM na kujiunga na Upinzani mwezi wa nane mwaka 2015. Nilipotoka CCM niliita press conference na nilioeleza wazi kwanini natoka CCM ns niliweka wazi kuwa natoka CCM kwa manufaa ya nchi na CMCM yenyewe. wakati natoka ccm nilikuwa mwanachama wa kawaida asiyekuwa na cheo chochote hata sikuwa mjumbe wa kamati yoyote au mwakilishi wa aina yoyote katika chama,” ameongeza Sumaye.
“Wakati wa kampeni baadhi ya viongozi wa CCM walidiriki kusema “huyu Sumaye dawa yake ni kumfilisi kwa kumnyanga’nya mashamba” hayo yalisemwa wazi na yaliandikwa katika baadhi ya magazeti , ninyi hapa ni mashahidi.”
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment