Neno la Alikiba baada ya kutajwa kati ya vijana 100 wenye ushawishi Afrika

Baada ya msanii wa Bongo Fleva, Alikiba kutajwa kuingia katika orodha ya vijana 100 wenye ushawishi Afrika 2017, ameelezea furaha yake.

“Najisikia vizuri kwamba Africa nzima imekutambua, kuna watu ambao wanatamani kuwa kama Alikiba na vitu kama hivyo. Kwa hivyo nawahamasisha vijana wengine kufanya kazi nzuri kama mimi nivyofanya, nashukuru sana, najisikia vizuri,” ameiambia The Playlist ya Times Fm.
Vijana wengine wa kitanzania waliotajwa katika orodha hiyo iliyotolewa na African Youth Awards  ni pamoja na Nancy Sumari, Diamond Platnumz, Elizabeth ‘Lulu’ Michael, Flaviana Matata, Millard Ayo na Jokate.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.