Sababu ya Jacqueline Wolper kuja na App yake

Msanii wa Filamu Bongo Jacqueline Wolper ameeleza sababu za yeye kuamua kuja na App.

Wolper atakuwa msanii wa pili kutoka katika tasnia ya filamu kufanya hivyo baada ya Wema Sepetu. Akipiga stori na Social Buzz ya Clouds Tv Wolper amesema moja ya sababu ni kuwa karibu na mashabiki zake na kuwaepusha kupata taarifa za uongo kuhusu yeye.

“Yeah ni kweli nataka kuja na App yangu na sababu kubwa ambayo imenifanya niwe na App ni kwa sababu mashabiki wengi wanatamanigi kujua vitu vyetu kwa undani kwa sababu wanakutana na facebook fake, wanakutana na mastori fake kwa hiyo ukiwa na App ni kitu kikubwa zaidi kuwaweka mashabiki zako karibu,” alisema Wolper.
Pia ameongeza kuwa “Kuchart nao kuwajibu maswali yao na chochote ambacho wanakisikia wewe unawanyooshea maelezo”.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.