SHILOLE AMCHANA HAMISA MOBETTO, ASEMA HANA UVUMILIVU NA MAMBO YAKE

Staa wa ngoma ya Kigoli, Shilole ameamua kutoa ya moyoni kuhusu habari inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na Diamond Platnumz na Hamisa Mobetto ambaye mtoto wake amempa jina Abdul Naseeb na hivyo kuwafanya watu waziamini tetesi kuwa amezaa na staa huyo wa Eneka.

Akipiga story na Dizzim Online, Shilole amesema Hamisa hana uvumilivu kwenye mambo yake na hakuwa na sababu ya msingi ya kupeleka mambo Instagram.
“Mimi sidhani kama kulikuwa na umuhimu wa kila kitu kukitangaza, vitu vingine vilitakiwa kukaa tu kimya kwasababu sidhani kama wazazi wetu wangekuwa wanafanya mambo hayo sidhani kama wangeweza kuishi na watu unakuja kujua ukweli baadaye so haikuwa na ulazima wa kila mtu kujua vitu vinavyoendelea,” amesema.
Aidha aliongeza na kusema, “Lakini muda mwingine inatokana na malezi huwezi kujua mwenzetu amelelewa vipi ya kutokuwa na uvumilivu na laiti ningekuwa mimi ningenyamaza tu kimya, nisingewafaidisha watu ukweli naujua mimi na Mungu wangu.”
Bado Diamond hajakubali kama mtoto wa Hamisa ni wake.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment