Shilole Amtambulisha Mchumba wake

Msanii Shilole amewaka wazi kuwa alikutana na mchumba wake kwa mara ya kwanza katika birthday ya Linah iliyofanyika Zanzibar.

Shilole na mchumba wake
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Kigori’, ameiambia Ala za Roho ya Clouds Fm kuwa walipokutana katika sherehe hiyo hakudhani kama wanaweza kuwa wapenzi lakini baadae ikaja kuwa hivyo.
“Nimekutana na Ashraf kwenye birthday ya Linah ilikuwa Zanzibar mwaka huu kwenye mwezi wa pili/kwanza, sikujua kama anaweza kuwa mpenzi wangu. Ni kijana tu ambaye alikuwa mtaratibu na mara nyingi alikuwa akinijali sana lakini naona kama nastahili kujaliwa kwa sababu mimi ni superstar lakini ndani ya moyo wake nilipokuja kugundua alikuwa ananipenda sana,” amesema na kuongeza.
“Ni mtu ambaye alikuwa anataka awe na mimi lakini anasindwa kuanza kwa sababu vitu hivyo vinakuwa vigumu kumuelezea mtu kama hujamzoea,” amesisitiza.
Wawili hao wamezidi kusisitiza kuwa mwaka huu mwishoni watafunga ndoa na mipango ya awali imeshafanyika.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment