Tamaa ya maisha mazuri bila kupiga kazi ni tatizo – Dkt Kigwangalla

Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangalla amesema kuwa tamaa ya maisha mazuri bila kupiga kazi ni tatizo jingine huku akisema vijana wengi wanafeli kwenye maisha kwa kupenda kuishi maisha yasiyo na uhalisia.

Dkt Kigwangalla ametweet katika ukurasa wake wa twitter ambapo alikuwa akijibu baadhi ya Watanzania wanaotumia mtandao huo kuhusu tabia ya vijana kutopenda kujishughulisha na kuchagua kazi.
“Kama mapambano ni makali zaidi sasa tunapaswa tuandae nguvu na mbinu kali za kiwango cha ukali uliopo, siyo kukata tamaa, Na huo ndiyo mwanzo wa tofauti ya waliofanikiwa na wasofanikiwa, kusimama kwenye uhalisia ama kuleta ubishoo kwenye kazi”, alitweet Dkt. Kigwangala.

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment