Tamasha la Fiesta lazinduliwa Dar, kuzunguka katika mikoa 15


Tamasha la Fiesta ambalo huvutia umati mkubwa wa watu kutoka sehemu mbalimbali nchini, limezinduliwa rasmi Jumatatu hii jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Fiesta, Sebastian Maganga (kushoto), Mtangazaji wa Clouds FM, Adam Mchomvu (katikati) pamoja Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa Tigo, William Mpinga.
Tamasha hilo ambalo huandaliwa kila mwaka na Kampuni ya Prime Time Promotions, mwaka huu linatimiza miaka 16 tangu kuanzishwa kwake. Linatarajiwa kufanyika katika mikoa 15 ambapo Watanzania watapata burudani na elimu jinsi ya kukabiliana na changamoto za maisha.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika makao mkuu ya Kampuni ya Tigo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Fiesta, Sebastian Maganga alisema tamasha hilo safari hii litajulikana kwa jina la Tigo Fiesta 2017 Tumekusomaa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Fiesta, Sebastian Maganga na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa Tigo, William Mpinga
Alisema safari hii Fiesta msimu wa 2017 wamejipanga vilivyo kuhakikisha Watanzania wananufaika na tamasha hilo katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na: kupata burudani na elimu ili kuhakikisha ubora wake wa miaka 15 iliyopita haupotei.
“Lakini pia baada ya uzinduzi huu, zoezi la usajili wa wasanii watakaoshiriki katika tamasha hilo unaanza mara moja na utachukua kama wiki mbili hivi, baada ya hapo ndipo itakapofahamika ni mkoa gani Tigo Fiesta 2017 Tumekosomaa itaanzia,” alisema Maganga.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment