Uchaguzi Kenya: Matokeo ya awali Kenyatta aongoza, Odinga apinga

Bado matokeo yanendelea kutangazwa kufuatia uchaguzi uliofanyika siku ya jana, nchini Kenya wa kuchagua Rais wa nchi hiyo na viongozi mbali mbali.

Mpaka sasa Rais Uhuru Kenyatta kutoka muungano Jubilee anaongoza kwa kura 6,574,087 sawa na (55.21%) akifuatwa na Raila Odinga kutoka muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) akiwa na kura 5,236,724 (43.98%).
Matokeo hayo ni ya vituo 31947 kati ya 40,883 ambapo kura 307,252 zimeharibika mpaka sasa hii ni kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kenya (IEBC).
Hata hivyo mgombea kutoka muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance (Nasa) Raila Odinga, ameendelea kuyapinga matokeo hayo yanayotolewa na IEBC.
Akiongea na waandishi wa Habari Odinga ameeleza kuwa tume hiyo imekuwa ikitangaza matokeo kwenye tovuti yake bila kufuata utaratibu unaofaa, ikiwemo kuwapatia mawakala wa Fomu 34A kutoka vituoni ili kubaini matokeo hayo yanavyo kwenda lakini wamekuwa akitangaza bila kufanya hivyo.
Haya ndio Matokeo yaliyotangazwa Alfajiri ya leo na Tume ya uchaguzi Kenya
1. Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 6,574,087 (55.21%)
2. Raila Odinga wa ODM kura 5236724 (43.98%)
3. Joseph Nyagah (huru) 29163 (0.24%)
4. Abduba Dida wa ARK 23318 (0.2%)
5. Ekuru Aukot wa Thirdway Alliance 20700 (0.17%)
6. Japheth Kaluyu (huru) 8806 (0.07%)
7. Cyrus Jirongo wa UDP 8521 (0.07%)
8. Michael Wainaina (huru) 6519 (0.05%)
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment