Amber Lulu adai Amber Rutty kamzidi kwa picha za utupu

Msanii wa Bongo Flava na video vixen, Amber Lulu amedai anachokifanya sasa video vixen mwenzie Amber Rutty katika mitandao ya kijamii kwa kuachia picha za utupu hata yeye kinamshtua.

Amber Lulu ambaye sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Only You’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa licha kile anachokifanya mwenzie kumshtusha, hawajawahi kuwa na beef kama watu wanavyodhani.

“Namjua nilishakutana naye mara moja tukasalimiana fresh, mtu mpaka kafanya hayo yote ina maana ananikubali haina haja ya kumkasirikia mtu, huwezi kuwa wewe kila siku,” amesema.
“Siyo nimemu-inspire kupiga picha za utupu, sema yeye anafanya hadi anazidi mpaka mwenyewe nilikuwa nashtuka, siku moja nikamtumia ujumbe Instagram fanya lakini jitahidi kidogo kujistiri, mimi mwenyewe sijawahi kufanya hivyo,” ameongeza.
Wiki iliyopita katika mtandao ilivuja picha ya utupu ya Amber Lulu na Young Dee kitendo kilichopelekea kukamatwa na Young Dee na kupelekwa polisi kwa madai yeye ndiye alivujisha picha hiyo, hata hivyo amekuwa akikanusha madai hayo.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment