Ebitoke afunguka Ben Pol kumzingua, ‘hapokei simu, hajibu sms’

Mchekeshaji Ebitoke amesema kwa sasa hayupo katika mahusiano mazuri na Ben Pol.
Wawili hao ambao walitangaza kuwa mapenzini miezi kadhaa iliyopita baada Ebitoke kujitokeza hadhara na kueleza anampenda mkali huyo wa muziki wa RnB Bongo, Ben Pol na hatimaye kuwa pamoja, kwa Siku za hivi karibuni hawajaonekana pamoja kama ilivyokuwa mwanzo.

Ebitoke ameeleza kuwa kwa sasa Ben Pol amekuwa akimpuuzia kwa mambo kadhaa hasa katika suala zima la mawasiliano.
“Simuelewi Ben Pol, simu hapokei, text hanilibu, ananipuuzia sijui kwanini” amesema Ebitoke. Hata hivyo ameenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa suala hilo linamuumiza sana kwani walikuwa na malengo makubwa sana.
“Hawezi kunichomoka kwa sababu tulipanga kabisa malengo na nitaendelea kuyapigania,” amesema.
Ameongeza kuwa wakati wanaanza uhusiano wao Ben Pol alikuwa single hivyo hana wasi wasi iwapo anafanya hivyo kutokana na mahusiano aliyokuwa nayo hapo awali.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment