Hatukatazi watumishi wa afya kumiliki maduka ya dawa – Waziri Ummy

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema serikali haikatazi watumishi wa afya kumiliki maduka ya dawa ni vizuri wakazingatia kuweka maduka hayo mbali na vituo vya afya.

Akizungumza wakati wa uzindua wa Ugawaji wa vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam . Ambapo alisema kuwa vituo vyao binafsi vya afya visiwe karibu na vituo hivyo ili kuepuka kutanguliza maslahi yao binafsi katika kutoa huduma za dawa kwa wagonjwa.
“Kuna changamoto nyingine kubwa badala ya kuandika dawa zile ambazo zipo kwenye orodha hawaandiki wanaandika dawa zao sisi hatutumii brand medicine sisi tunatumia generic medicine kama umeandikiwa amoxlin ipo kuna aina ya dawa zaidi ya tano ya antibioyotic utamwambiaje akanunue kwenye duka naomba niseme kivingine Mkuu wa wilaya mna vyombo usipoangalia vizuri haya maduka ni ya kwetu sisi,” alisema Waziri Ummy.
“Hatusemi watumishi wa afya wasimiliki maduka ya dawa lakini pia tuangalie wapi tutachora mstari hizi dawa za serikali na hizi sio dawa za serikali hatukatazi narudia tena hatukatazi watumishi wa afya wasimiliki maduka ya madawa lakini unaweza kuta palepale nje ya hospitali unakuta duka la mfanyakazi hatuwezi kukubali.”
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment