Makamu wa Rais akiri kuchepuka nje ya ndoa

Makamu wa Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, amekiri wazi kuwa na mchepuko nje ya ndoa miaka 8 iliyopita lakini amekana taarifa zinazosambaa nchini humo kuwa anawapenzi wengi huku akidai taarifa hizo zina lengo la kumchafulia jina.

Makamu wa Rais nchini Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.
Bwana Ramaphosa amesema anaamini kuwa taarifa zinakuzwa ili kumuharibia mipango yake ya kugombea urais kupitia Chama The African National Congress (ANC), wakati Rais Jacob Zuma atakapong’atuka madarakani.
Taarifa kutoka Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) zinasema kuwa wadukuzi walidukua mawasiliano yake kwa njia ya barua pepe ili kuthibitisha uhusiano wake wa siri nje ya ndoa na daktari mmoja nchini humo.
Kwenye mahojiano yake na gazeti la Sunday Independent la nchini Afrika Kusini, Bwana Ramaphosa amekiri kuwa na mwananmke nje ya ndoa miaka nane iliyopita ila taarifa za sasa zina lengo la kumchafulia jina huku gazeti hilo likieleza kuwa lilikatazwa na Ramaphosa kuchapisha e-mail zilizodukuliwa.
Cyril Ramaphosa ana mke na watoto wanne na ni mfanyabiashara mkubwa na ni moja ya viongozi wenye ushawishi ndani ya Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC, na ana nafasi kubwa ya kumrithi Rais Jacob Zuma, kwenye uchaguzi ujao.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment