Mhe Kigwangalla ataja njia mbadala ya kukabiliana na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume

Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangalla amesema kuwa kwa sasa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume nchini limekuwa kubwa ingawaje hakuweka wazi kutokana na usiri wa tatizo hilo huku akiwataka wanaume kuzingatia mlo bora na kufanya mazoezi.

Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla
Mhe Kigwangalla akijibu swali jana bungeni lililoulizwa na Mbunge wa Konde, Mhe Khatib Haji likihoji “Kumekuwa na ongezeko kubwa kwa tatizo la wanaume kupungukiwa nguvu za kiume Je, Serikali inajua tatizo hilo? na kama inajua inachukua hatua gani kukabiliana na tatizo hilo?”.
Napenda kutoa hamasa kwa wanaume wote nchini, kushiriki kwa kiasi kikubwa kwenye mambo yanayolinda afya zetu, kufanya mazoezi, kupumzika, kula vizuri lakini pia kufurahi, kucheka na kushirikiana na wenzako ili kuondoa msongo wa mawazo kwasababu msongo wa mawazo, sonono  wasiwasi ni katika vitu vinavyosababisha Erectile disfunction na hata kukosa watoto kwa wengine kushindwa kushika mimba…Naamini tukizingatia tutaweza kukabiliana na tatizo hilo“,amesema Dkt Kigwangalla.
Hata hivyo, kwa upande mwingine Waziri Afya, Mhe Ummy Mwalimu ametoa tamko kuwa watu wote wanaouza dawa za kuongeza nguvu za kiume kufuata taratibu za vibali maalumu kutoka Mamlaka ya Dawa na Chakula (TFDA) na TBS.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.