Mhe Nyalandu aomba kumsafirisha Tundu Lissu Marekani

Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameweka kambi nchini Kenya kuangalia uwezokano wa kupata ruhusa kutoka kwa madaktari ya kumsafirisha Mh Tundu Lissu kwenda Marekani kwaajili ya matibabu zaidi baada kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.

Nyalandu amedai ni siku ya tatu bado hajapata ripoti inayoonyesha maendeleo ya mgonjwa huyo ili waangalie kama wanaweza kwenda nchini Marekani kwaajili ya matibabu zaidi.
Taarifa ya Mh Nyalandu
Tumekuwa #NairobiHospital tukisubiri MADAKTARI watoe RIPOTI ya mwenendo wa MATIBABU ya Mh #TunduLissu kwa minajili ya kuwapatia MADAKTARI BINGWA wa Marekani na kuona uwezekano wa Mh #TunduLissukupatiwa RUFAA kwa matibabu zaidi NJE., LAKINI bado KALAMU zao ni nzito kuandika RIPOTI hii siku ya tatu tangu tuahidiwe. Binafsi, nimerudi NAIROBI tangu JANA kushiriki maandalizi ya uwezekano wa kumhamishia Mh #TunduLissu Marekani kwa ajili ya huduma yenye ubora zaidi, endapo MADAKTARI wa #NairobiHospitalwangeridhia. Kesho asubuhi nitarejea hospitalini kusikiliza kauli ya mwisho ya MADAKTARI kuhusu RIPOTI hiyo.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment