Mhe. Spika nashukuru kwa msamaha wako wa bure – Lema


Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema amemshukuru Spika wa Bunge la Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kwa kumsamehe baada ya kuzungumza maneno aliyokuwa akimlalamikia Spika kuhusu michango ya Tundu Lissu.

Lema ametumia ukurasa wake twitter leo kuandika ujumbe huo huku akisema yeye na familia yake wamechagua kuendelea kumuombea.
Leo Bungeni Mhe. Spika ameonyeshwa kuchukizwa na tuhuma hizo ambapo amewaeleza Wabunge jinsi alivyosononeka na anavyozidi kusononeshwa.
“Unatulaumu jambo gani ndugu yangu Spika angefanya nini na ndio huu mshahara naupokea kutoka kwenu kila siku hivi kweli ndugu zangu mkoje nyinyi ni watu wa Mungu au watu wa nani wagonjwa wangapi wameugua hapa wabunge mliwahi kumchangia mgonjwa yupi wengine wamekufa tumewasindikiza hapa wakina Mzee Sitta tumewaleta hapa nani aliwahi kuchangiwa lakini nikawashawawishi kuna wengine walikuwa hawataki humu milioni 43 ikamsaidie mwenzetu mshahara wetu huo, anachangisha wabunge Mhe. Spika tungefanyaje uwezo wetu ndio huo,” alisema Spika Ndugai.
“Lakini leo hii tukiambiwa Mhe. Lissu anapelekwa India sasa katika utaratibu wetu ule tutachukua gharama wala haina tatizo mradi tu Waziri Mkuu akishaniambia na nini wala haina shida kwasababu utaratibu wetu sisi ndio huo haina sababu ya mambo kama haya kwa hiyo tuwe tunaona aibu mimi ndugu zangu upinzani muwe mnakaa pamoja katika hili ndugu yetu muwe na utaratibu huo msibebane tu kwa kila jambo kwa hili fasheni nikumtuhumu Spika fasheni ni kulidharau Bunge fasheni ni kufanya hivi kwa jinsi nilivyosononeshwa na ninavyoizdi kusononeshwa na baadhi ya maneono ya nyinyi watu “kweli huyu namsamehe tu ajui atendalo na wote si tumsamehe tu bwana huyu eeh kw watu wa Arusha niwaambie tu niwaambie neno moja tu la Kiingereza Arusha deserves better,” aliongeza Spika.
Kwa upande wake Mbunge huyo wa Arusha Mjini (CHADEMA) ameandika hivi: Mh Spika nashukuru kwa msamaha wako wa bure , lakini Mimi na familia yangu tumechagua kuendelea kukuombea .
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment