Si rahisi serikali kuagiza tohara kuwa lazima kwa wanaume – Dkt Kigwangalla

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa si rahisi kwa serikali kuagiza tohara kuwa lazima kwa wanaume wote nchini japo kuwa tohara ina faida kubwa sana kiafya kwa wananchi.


Dkt Kigwangalla maeyazungumza hayo leo Bungeni mjini Dodoma, wakati akijibu hoja za wabunge bungeni ambapo amesema kuwa wizara yake iliweka mikakati ya kubaini mikoa ya kipaumbele ambayo haina utamaduni wa kutahiri.  “Si rahisi kwa serikali kuagiza tohara kuwa lazima kwa wanaume wote nchini japokuwa tohara ina faida kubwa sana kiafya kwa wananchi wetu wizara iliweka mikakati ya kubaini mikoa ya kipaumbele ambayo haina utamaduni wa kutahiri na ina kiwango kikubwa cha Virusi Vya Ukimwi na kutoa huduma ya tohara kama hafua rasmi mikoa hiyo ni 14 Iringa, Njombe, Tabora, Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi Ruvuma Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Geita, Kagera na Musoma itakapo fikia mwzi Oktoba mwaka 2017 mikoa mipya minne ambayo ni Singida , Kigoma, Mara na Morogoro itaongezwa na hivyo kufikisha idadi ya mikoa 17,” amesema Kigwangalla.  “Elimu kuhusu tohara imefikishwa kwa kiasi kikubwa ambapo serikali kwa kushirikiana na wadau wake katika mikoa ya kipaumbele imekuwa ikitoa elimu kabla na baada ya huduma ya tohara katika vituo vya kutolea huduma za afya na wakati wa huduma mkoba zinazotolewa katika ngazi ya jamii kupitia kampeni mbalimbali serikali ilianzia kampeni maarufu iitwayo ‘MKONO DONDOSHA SWETA‘ ambapo elimu kuhusu tohara ilitolewa kupitia matangazo na vipindi vya redio na televisheni, mambango , machapisho, vijarida mbalimbali, filamu na waelimisha rika.”
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment