Sitanyamaza – Peter Msigwa

Baada ya Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema) kukamatwa akiwa kwenye Mkutano wake wa hadhara na kuachiwa kwa dhamana amesema kuwa polisi hawezi kumpangia nini cha kusema na hatanyamaza.

Mbunge huyo amedhaminiwa na wadhamini wawili akiwepo Mwenyekiti wa Bavicha Iringa, Leonce Marto amesema kuwa wamemkamata akiwa anatimiza majukumu yake ya kibunge.
Mbunge huyo kupitia mitandao yake ya kijamii ameandika hivi:
Polisi hawawezi kunipangia nini cha kusema na wala sio majukumu Yao. Wamenikamata nikitimiza majukumu yangu ya kibunge! SITANYAMAZA!
Msigwa alishushwa jukwaani akiwa anahutubia mkutano katika kata ya Mlandege Manispaa ya Iringa huku akituhumiwa na kosa la uchochezi dhidi ya vyombo vya usalama .
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment