Tundu Lissu apigwa risasi Dodoma, akimbizwa hospitali

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu amekimbizwa hospitali mchana huu baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana leo mchaa akiwa nyumbani kwake Mkoani Dodoma.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa Mh. Lissu amepigwa risasi zaidi ya mbili alipokuwa ametoka bungeni na kwenda nyumbani kwakwe kwa ajili ya chakula cha mchana.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba amekimbizwa hospitali na sasa yupo chumba cha upasuaji.
Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa ajili ya kufahamu taarifa zaidi.

Kwa upande wa mwanasiasa wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe Ruyagwa‏ amewataka watanzania kuendelea kumuomba mwanasiasa huyo ambaye ni Mbunge wa Singida.

“Tumwombee Tundu Lissu. Kila mtu aombe Kwa imani yake. Mungu ampe nafuu inshallah,” alitweet Zitto.
Source: EATV
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment