Tuweke pembeni tofauti zetu, Tundu Lissu ameumizwa vibaya – Mhe Lazaro Nyalandu

Juzi Jumamosi ya tarehe 16 septemba 2017, Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Mhe Lazaro Nyalandu alienda nchini Kenya kumjulia hali Mbunge mwenzie wa Jimbo la Singida Mashariki, Mhe Tundu Lissu aliyejeruhiwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana wiki mbili zilizopita mkoani Dodoma.

Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Mhe Lazaro Nyalandu
Mhe. Nyalandu baada ya kibali kupata ruhusa ya kumuona Tundu Lissu amesema hali yake inaendelea vizuri na ameongea nae huku akiweka wazi kwa watu ambao hawajapata nafasi ya kumuona kuwa Mbunge huyo aliumizwa vibaya sana na risasi.
Nimeonana na Mh. #TunduLissu katika chumba chake hospitali ya Nairobi na kuzungumza naye kuhusu hali yake na anavyoendelea.UKWELI ni kwamba, ameumizwa vibaya. Imeelezwa kwamba MADAKTARI wanaendelea na hatua kadhaa za matibabu, wakiwa wameanza kwa kumuimarisha (stabilization), ili kuufanya mwili uweze kumudu hatua zaidi za utibabu anazopaswa kufanyiwa. AIDHA, katika kuongea naye, Mh. Lissu ameonesha uso wa tabasamu, huku akimshukuru MUNGU kwa kumruhusu kuwepo hai. NAAMINI kwamba hatua zaidi na za haraka zitahitajika kumsaidia apate huduma za kitabibu katika ubora na ufanisi uliopo kwa sasa duniani.“ameandika Mhe Lazaro Nyalandu kwenye ukurasa wake wa Facebook mapema jana baada ya kuonana na Lissu, huku akiwataka Watanzania kuweka pembeni tofauti zao za kiitikadi na kuendelea kumuombea apone haraka.
Ni maombi yangu kwetu SOTE , tuweke pembeni tofauti zetu za kiitikadi, ama mitazamo, tuungane na kushikamana kama Taifa kwa ajili ya kumwomba MUNGU anyooshe mkono wake, na kumponya. HALIKADHALIKA, SOTE tuungane kutoa msaada wa hali na mali kwa kadri ya uhitaji wake. AMANI iwe naye!“ameandika Lazaro Nyalandu.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment