Chuo kikuu cha Nairobi chafungwa

Nairobi, Kenya. Chuo Kikuu cha Nairobi kimefungwa kwa muda usiojulikana.
Wanafunzi chuoni hapo waliamriwa ifikapo saa tatu asubuhi leo Jumanne wawe wameondoka chuoni hapo.

Uamuzi huo umefikiwa na Seneti ya chuo kutokana na suala la kiusalama.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Umma wa chuo hicho, John Orindi amesema, “Tutatangaza ni lini chuo kitafunguliwa.”
Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na maandamano yaliyofanyika wiki iliyopita ambayo yalisababisha wanafunzi 27 kujeruhiwa.
Chanzo: Mwananchi

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment