DIAMOND PLATNUMZ ASEMA NENO KUHUSU MAROMBOSO KUINGIA RASMI WCB WASAFI

Staa wa muziki wa Bongo Fleva na mmiliki wa lebo ya muziki ya WCB Wasafi, Diamond Platnumz amemaliza utata wa kilichokuwa kikisemekena chini kwa chini kuhusu mmoja kati ya wasanii waliounda Bendi ya Yamoto ‘Maromboso’ kudaka dili la kufanya kazi chini ya Usimamizi wa leo ya WCB Wasafi.
Kupitia ukurasa wa Instagram katika kumtakia heri ya tarehe ya mfanano wa siku ya kuzaliwa kwa Maromboso, Diamond amethibitisha kuwa ni muda muafaka tu unaosubiriwa kubayanisha kuwa muimbaji Maromboso atafanya kazi rasmi kama msanii chini ya usimamizi wa lebo kama inavyofanyika kwa wasanii wengine kama vile Rich Mavoko, Harmonize, Lava Lava, Ray Vanny na Queen Darleen.
Taarifa ambazo hazikuwa na uhakika kuhusu Maromboso kuanza kufanya kazi na lebo ya muziki ya WCB Wasafi zilianza kukolea zaidi kipindi ambacho Kundi la muziki la Yamoto Bendi lilipoanza kuingia katika sura ya kuvunjika kwa mfumo wa kila msanii aliyeunda Bendi hiyo kufanya kazi zake binafsi ambapo baadae Maromboso alitokea katika wimbo wa ‘Zilipendwa’ uliowashirikisha wasanii wote wa lebo ya WCB huku amshabiki wengi wao walijijazia majibu wenyewe kuwa Maromboso ameanza kufanya kazi na lebo hiyo


Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment