Gharama za matibabu ya Mh. Lissu zatajwa

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Taifa, Mh. Freeman Aikaeli Mbowe amesema gharama za matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyeshambuliwa septemba 7 kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika eneo la ‘area D’ Dodoma zimefika sh. milioni 412.7.

Mbunge Lissu ambaye anapatiwa matibabu katika hospitali ya Aghakan nchini Kenya ambapo ameeleza kuwa mpaka sasa mbunge huyo amefanyiwa operation saba.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Makao makuu ya chama hicho yaliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, Tanzania amesema kuwa hali ya mbunge huyo imeimarika na vifaa vyote vilivyokuwa vikisapoti mwili wake vimeondolewa kwa kuwa kwasasa mwili wake unaweza kujitegemea.
“Jumla ya matibabu mpaka mimi ninapotoka Nairobi yafikia milioni 417. 7, tunashukuru sana wabunge wa Chadema na vyama vingine kikiwemo CUF, ACT- Wazalendo, CCM. Tunaishukuru sana familia ya Lissu, imekuwa na msimamo kama Lissu mwenyewe. Tumefanya kazi na familia na tutaendelea kufanya kazi na familia. Tutakapokwenda katika matibabu ya tatu, tutaiacha kwa familia iwe msemaji wa kwanza, mgonjwa anaweza kuongea na kujitambua,” amesema Mbowe.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amewashukuru watu waliokuwa wakihamasisha michango hiyo akiwemo Mange Kimambi na Wema Sepetu ambapo kupitia Watanzania walio nje ya nchi wamechanga kupitia Go fund me Dola 29,000 za Marekani.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment