Hamisa Mobetto Kala deal la Diamond na Zari ?????

Mwanamitindo Hamisa Mobetto huwenda akawa umeingizwa kwenye deal la matangazo la kampuni ya GSM ambalo pia, Diamond na Zari yupo ndani.

Hamisa Mobetto

Miezi sita iyopita Diamond na mama watoto wake, Zari The Bosslady walionekana kwenye tangazo la pamoja la vifaa vya ndani vya kampuni ya GSM. Katika tangazo hilo Zari alionekana akitambulishwa katika nyumba mpya ya Diamond ambapo mrembo huyo wakati anatambulishwa alikuta hereni katika nyumba hiyo.
Tetesi ambazo zilikuwa katika mitandao ya kijamii kwa wakati huo ni kwamba wawili hao waligombana baada ya Zari kukuta hereni chumbani kwa Diamond huku wadau wa mambo wakidai hereni hizo zilikuwa za Hamisa Mobetto.
Sasa Jumapili hii, Hamisa Mobetto ameligusia suala hilo la hereni huku wadau wa mambo wakidai mrembo huyo atakuwa amekula shavu kutoka kampuni ya GSM.
“It’s about time nifate hereni zangu @danubehometz_ I hope they are still there!๐Ÿ’ƒ๐Ÿฝ,” aliandika Instagram Mobetto kupia video hapo chini.


A post shared by HamisaMobetto (@hamisamobetto) on
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment