Hukumu ya kesi ya Lulu kusomwa Novemba 13 mwaka huu (+Video)

Kesi inayomkabili muigizaji wa Filamu,  Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo alhamisi imeendelea kusikilizwa Mahakamani ambapo washauri watatu (Wazee) wa Mahakama Kuu wamesema mshitakiwa Lulu aliua bila ya kukusudia.

Washauri hao wametoa maoni yao leo Alhamisi Oktoba 26,2017 baada ya upande wa Jamhuri na wa utetezi kukamilisha kuwasilisha ushahidi.
Muigizaji, Lulu ambaye yupo nje kwa dhamana anakabiliwa na kesi ya kumuua aliyekuwa muigizaji wa filamu, Steven Kanumba bila kukusudia.
Lulu anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7,2012, nyumbani kwa Kanumba, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam. Jaji Sam Rumanyika amesema hukumu itatolewa Novemba 13, 

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.