Kesi ya Lulu ya kuua bila kukusudia yanguruma Mahakama Kuu

Kesi inayomkabili Diana Elizabeth Michael (LULU)  ya kuua bila kukusudia imeanza kusikilizwa Alhamisi hii Mahakama Kuu chini ya jaji Sam Rumanyika.
Mrembo huyo wa filamu anakabiliwa na kesi ya muua aliyekuwa mpenzi wake, Steven Kanumba tukio linalodaiwa kufanyika mwezi Arpili mwaka 2012.

Shahidi wa kwanza wa upande wa Jamhuri, Seth Bosco ambaye ni mdogo wake Kanumba amesema siku ya tukio Kanumba alimwambia asitoke kwa madai siku hiyo walikuwa watoke wote.
Shahidi huyo ambaye alikuwa anaishi na Kanumba, Sinza Vatcan kwa kipindi kisefu, amedai siku ya tukio kaka yake huyo alikuwa yupo katika hali nzuri.
Seth amesema usiku wa siku hiyo yaani sita usiku aliingia Lulu na baada ya muda mchache alisikia kelele za Lulu na Kanumba wakigombeana simu ya mkononi.
Shahidi wa pili ambaye alikuwa asikilizwe leo amepata hudhuru hivyo kesi hiyo itaendelea kusikilizwa siku ya kesho.
Kwa mujibu wa ripoti ya Daktari, Kanumba anadaiwa kuwa alifariki baada ya kukosa hewa kwenye Ubungo.
Waliki wa upande wa Jamhuri ni Faraja George.
Lulu alifika mahakani hapo akiwa pamoja na ndugu jamaa na marafiki.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.