Lady Jaydee na Mwana FA wamaliza bifu lao

Hawajui tulipotoka, watajuaje tunapokwenda? Ya kwao yanawashinda yetu hawataweza – Hayo ni mashairi ambayo Lady Jaydee ameimba katika wimbo ‘Hawajui’ wa Mwana FA ambao umetoka zaidi ya miaka tisa iliyopita.
Wimbo huo ulifanya vizuri sehemu mbalimbali na kuteka mashabiki wengi zaidi. Hata hivyo stori ya Jaydee na Mwana FA ya kuwa kama kaka na dada ghafla ikageuka na kuwa kama paka na panya.
Wawili hao wamedumu kwa miaka kadhaa wakiwa katika ugomvi mzito ambao wengi wao hawajui chanzo chake. Jumanne hii mashabiki walipatwa na mshtuko mkubwa baada ya kuona FA kupitia mtandao wake wa Instagram amepost video ya wimbo mpya wa Jide ‘I Miss You’ na kuandika, “Lady JayDee new music video ” I Miss You” is finally out . Click link in her bio @jidejaydee , watch share and enjoy!karibu…”
Wakati huo huo Jaydee na yeye ame-comment kwenye video hiyo na kuandika, “More blessings ๐Ÿ™๐Ÿฝ✌๐Ÿฝ&๐Ÿ’™.” sio mashabiki pekee ambao wameonekana kufurahia tukio hilo, wengine ni mastaa wakubwa hapa Bongo akiwemo Professor Jay na Ambwene Yessaya (AY).
Mwenye macho haambiwi ona, kutokana na tukio hilo inaonyesha kuwa wawili hao tayari wameshayamaliza matatizo yao. Hata hivyo bado mashabiki wengi wamekuwa wakitamani kuwasikia wasanii hao tena wakifanya wimbo wa pamoja kama walivyowahi kufanya kwenye ngoma tatu zilizopita, je tutegemee hjilo linaweza kutokea tena?

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment