Maneno ya Mbunge Nape baada ya kusikia sauti ya Mh. Lissu ‘Tulia mjomba upone kabisa’

Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye baada ya kusikia sauti ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antiphas Lissu ambaye tangu alipopigwa risasi haijawahi kusikika sauti yake amemuomba mbunge huyo atulie mpaka apone kabisa.

Nape amesema anamuombea Mbunge apone kwanza  huku akisema anamshukuru Mungu kwa kuliona tabasamu lake.
Mjomba tunamshukuru Mungu kwa tabasamu hili la matumaini!Nakuombea afya iimarike kabla hujasema mengi!Tulia mjomba upone kabisa kwanza! ameandika Nape kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Hata hivyo, hivi  karibuni Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe alisema kuwa hali ya mbunge huyo imeimarika zaidi na vifaa vilivyokuwa vikiusapoti mwili wake vimeondolewa na sasa mwili wake unajiendesha wenyewe.
Mh. Lissu  alipigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 mwaka huu eneo la ‘area D’ mjini Dodoma na watu wasiojulikana. Ambapo kwasasa anapatiwa matibabu Nairobi Kenya.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment