Maoni ya wazee wa Baraza Mahakamani kwenye kesi ya Lulu

Alhamisi hii kesi ya Elizabeth ‘Lulu’ Michael inayomkabili ya kumuuwa muigizaji mwenzake Steven Kanumba bila kukusudia imeendelea katika Mahakama Kuu kwa wazee wa Baraza kutoa maoni yao juu ya kesi hiyo.

Katika maoni ambayo yametolewa na wazee watatu wa baraza hilo wote kwa pamoja wamesema kuwa wameidhishwa na ushahidi uliotolewa kwa pande zote na hivyo Lulu aliuwa bila kukusudia.
Mzee wa kwanza alitoa maoni yake kwa kusema kuwa, mshtakiwa (Elizabeth Michael) ameua bila kukusudia.
Naye mzee wa pili alitoa maoni yake kwa kusema, “Naweza kusema kuwa Elizabeth hakuua kimakusudi, aliua bila kukusudia.”
Wakati huo huo mzee wa tatu hakusita kuungana na wenzake waliopita kwa kusema, “Nimeridhika na ushahidi uliotolewa kwa pande zote mbili, Elizabeth ameua bila kukusudia Kutokana na marehem kuwa na mwili mkubwa.”
Hata hivyo Jaji amesema kuwa hukumu ya kesi hiyo itasomwa tarehe 13 Novemba ya mwaka huu.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.