Mh. Lissu aona jua kwa mara ya kwanza

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Taifa, Mh. Freeman Aikaeli Mbowe ameeleza kuwa hali ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu imeaimarika na ametoka ICU na kuona jua kwa mara ya kwanza tangu ashambuliwe na watu wasiojulikana Septemba 7 mwaka huu.

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mbowe amesema kuwa katika wagonjwa waliopelekwa katika hospitali hiyo, mbunge huyo ni wa kwanza kutumia damu nyingi zaidi katika miaka 20 iliyopita.
“Nataka niwaambie kuwa Lissu amefanyiwa upasuaji mara 17 mpaka sasa, ameongezewa damu nyingi kuliko mtu yeyote katika hospitali hiyo miaka 20 iliyopita ametoka ICU wiki iliyopita na ametolewa vifaa vyote vilivyokuwa vikisapoti mwili wake.Juzi kwa mara ya kwanza alikaa, anatembea Wheel Chair na aliliona jua kwa mara ya kwanza ,” amesema Mbowe.
Katika hatua nyingine Mbowe amesema kuwa Mhe. Lissu ataanza awamu ya tatu nje ya Nairobi kufanyiwa matibabu huku akieleza kuwa hawatataja sehemu hiyo ni wapi kwa sasababu ya usalama wa mbunge huyo.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment