Miss World 2017 ni ya kwetu kwa urembo huu wa Julitha

Hellow karibu katika habari za mitindo kutoka hapa Bongo5, na leo tunamuangalia mshiriki kutoka Tanzania, Julitha Kabete anayekwenda kuwakalishi taifa lake katika mashindano ya urembo wa dunia (Miss Word 2017) nchini China.

Mashindano hayo yatafanyika mji wa Sanya, ifikapo Novemba 18 mwaka huu na yatahusisha nchi zipatazo 120 kutoka pande tofauti za dunia. Tukimuangalia Julitha kuanzia urembo, mavazi na muonekano anastahiki kuwa Miss Word 2017 vile vile anaweza kuwa Miss Word Africa kwani mrembo huyo anavigezo vyote vya kushinda taja.
Ni muda mrefu Tanzania haijawahi kutoa Miss Word Africa, tangu mwaka 2005 Nancy Sumari aliposhinda taji hiyo.
Julitha amewahi kuwa Miss Africa Tanzania 2016, Climate Change Ambassador kutokana na sababu hiyo na sababu za kiurembo anavigezo vya kuweza kushinda shindano hilo, kwani ameishi katika mazingizara ya urimbwende na anauzoefu.Pia atakuwa nafaamu vizuri changamoto za mashindano na ninaamini amesha jiandaa vya kutosha kisaikolojia.
Hizi ni baadhi ya picha za mrembo:
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.