Mkwara mzito wa Barakah The Prince kuhusu Naj, ‘nitakuharibu sana’

Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Barakah The Prince amesema anapoachana na mpenzi wake ni lazima awe adui yake kwanza, hivyo wale wanaodai kuwa wameachana na mpenzi wake, Naj hilo halipo kwa sababu bado wapo pamoja.


Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Sometime’ ameiambia E-Newz ya EATV kuwa endapo ameachana na Naj watu wangejua tu kutokana na kasumba yake ya anapoachana na mtu kuwa adai yake.
“Mimi nikimwaga kila mtu atajua kwa sababu mwenzako, kwanza nataka nikimwaga uwe adui kwa hiyo nitakuharibu sana simwaganagi kwa amani, kwa hiyo kila mtu angejua ningetangaza siyo demu wangu, kwa hiyo kama siyo demu sinasema tu, kwani nimeshaachana na wangapi” amesema Barakah.
Katika hatua nyingine Barakah amesema mapenzi yake na Naj ni nyumbani siyo lazima kwenye mitandao, hivyo wale wanaosema kwanini sasa hivi hawapostiniani katika mitandao wanapaswa kuelewa kila mmoja anafanya muziki na ana mashabiki wake ambao wanataka kuona kazi zake tu na si picha/kazi za mwingine.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment