Mtangazaji wa E-Fm na Tv-E Dennis Rupia ‘Chogo’ amefariki dunia

Mtangazaji wa kituo cha redio cha E-Fm na TV-E cha jijini Dar es Salaam, Denis Rupia maarufu kwa jina la ‘Chogo’ ameaga dunia katika hospitali ya Lugalo alikokuwa anatibiwa usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa kipindi kifupi.

“Uongozi na wafanyakazi wa E-fm, TV -E kwa majonzi na masikitiko tunatangaza kuondokewa na mwanafamilia mwenzetu Dennis Rupia (Chogo) aliyefariki Dunia baada ya kuugua kwa kipindi cha muda mfupi. Tutaendelea kufahamishana taratibu za kumpumzisha mpendwa wetu kupitia vyanzo mbalimbali. Hakika ni kipindi kigumu kwetu, wasikilizaji wa Redio na familia kwa ujumla tuendelee kumuombea mpendwa wetu.”Imeeleza taarifa iliyotolewa na E-fm na TV-E.
Chogo alijizolea umaarufu kwenye segmenti ya Bakola kwenye kipindi cha Joto la Asubuhi na kipindi cha sakasaka na shika ndinga vyote vya TV-E, pamoja na jingle na matangazo lukuki ya kituo hicho.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment