MWANAMKE ALIYEDAI KUBAKWA NA NELLY ATAKA KESI IFUTWE

Mwanamke aliyedai kuwa amebakwa na rapper Nelly wa Marekani kwenye basi lake la ziara wikiendi iliyopita anataka mashtaka hayo yafutwe.

Mwanasheria wake, Karen Koehler alisema kwenye maelezo Ijumaa hii kuwa mteja wake hataki uchunguzi uendelee na hatokubali kutoa ushahidi.
Koehler anasema msichana huyo anatamani asingepiga 911 sababu anaamini mfumo wa sheria utamuangusha. Pia anasema ni ngumu watu kumuamini kwakuwa Nelly ni mtu maarufu na tayari anapata misukosuko mingi tangu habari hiyo isambae.
Polisi wa huko Auburn walimkamata Nelly Jumamosi iliyopita kwa madai ya kubaka. Hata hivyo aliachiwa bila kushtakiwa kwa kosa lolote.
Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.