Picha ya Lissu yamgusa Haji Manara

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instragram ameweka picha ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye kwa sasa yupo Jijini Nairobi nchini Kenya kwa matibabu nakuandika kuwa anamuombea apone licha ya kutokuwa shabiki wake wala chama chake cha siasa.


Haji Manara ambaye ni mwanachama wa CCM amesema hayo leo baada ya kuona picha ya kwanza ya Mbunge huyo wa Singida Mashariki, Tundu Lissu akiwa hospitali nchini Kenya ambapo anapatiwa matibabu kufuatia kupigwa risasi Septemba 7 mwaka huu na watu wasiojulikana.

“Ohhh God,,,mm sijawah kukushabikia ww wala chama chako,,ila nakuombea kwa Mungu upone haraka kaka,,urudi ktk harakati zako,,nikiamini bila uwepo wenu chama changu kitalala.”

Share on Google Plus

About mwanaidinuhu

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments/maoni:

Post a Comment